
Rais John Magufuli
RAIS John Magufuli leo tarehe 16 Julai 2019, ametoa zawadi ya magunia 15 ya mchele pamoja na ng’ombe watatu kwa wafungwa na mahabusu waliopo kwenye gereza kuu la Butimba, jijini Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Kiongozi huyo wa nchi yupo ziarani jijini Mwanza ambapo ametembelea gereza hilo. Hata hivyo, mahabusu hao walipata fursa ya kumweleza Rais Magufuli changamoto wanazokumbana nazo.
“Hapa (gerezani) ni kama mtakuja, mimi ni kama mfungwa mtarajiwa, uongo?” aliwahoji wafungwa na mahabusu aliowatembelea.
Baada ya kuwauliza wanakula kiasi gani kwa wiki, Rais Magufuli aliwaeleza wakuu wa gereza hilo kuwa atawapelekea ng’ombe watatu na magunia 15.
“Sasa siku hiyo chinjeni ng’ombe na mpike mle. Ni nyinyi askari pamoja na hawa vijana, kula pamoja kunajenga upendo,” amesema.
More Stories
Jamhuri yakwamisha kesi ya Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi
Sh54 Bil. kugharamia mradi wa maji Chiuwe
Serikali yapewa neno ununuzi treni zilizotumika