March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JPM: Wapinzani njooni niwatue mzigo

Mwita Waitara, Naibu wa Waziri wa TAMISEMI

Spread the love

RAIS John Magufuli amewakaribisha wabunge na madiwani wa upinzani wanaosumbuka na mizigo katika vyama vyao, kuingia CCM. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameyasema hayo leo tarehe 27 Septemba 2018 jijini Dar es Salaam wakati akifungua barabara ya juu (Fly Over) katika makutano ya barababara ya Nyerere na Tazara.

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wabunge wanaotambua na kuunga mkono juhudi za serikali akiwemo Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

“Ninawapongeza wabunge walioona mambo mazuri yanayofanywa na serikali akiwemo Waitara, sijasema wote waje siwahitaji, lakini wanaoguswa. Wanaosumbuka na mamizigo ya vyama vingine waje ninawakaribisha tuweze kujenga nchi yetu,” amesema.

error: Content is protected !!