December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli awaapisha Mawaziri na Manaibu

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amewaapisha Mawaziri na Manaibu waziri wapya Ikulu jijini Dar es salaam leo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Jumla ya Mawaziri na Manaibu waziri 32 wameapishwa huku hatima ya wizara zingine nne ikiwa bado haieleweki kitendawili chake kitatenguliwa lini.

Wizara ambazo bado hatima yake iko gizani ni Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Wizara ya Maliasili na Utalii,na Wizara ya Fedha na Mipango, Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano.

Baraza hilo jipya lina sura mpya zipatazo 17 huku baadhi ya wakongwe walio hudumu katika awamu iliyopita wakizua maswali miongoni mwa jamii.

Baadhi ya Mawaziri wanaotiliwa shaka ni wale ambao waliondolewa kwa kashfa katika serikali ya awamu iliyopita.

error: Content is protected !!