JOHN Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda mchache uliopita amewaapisha mawaziri wawili na manaibu wanne aliowateua siku ya Jumamosi tarehe 10 Novemba, 2018 kutokana na mabadiliko madogo aliyoyafanya katika baraza la mawaziri. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Waziri wa kwanza kuapa alikuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda na kufuatiwa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga.
Baada ya mawaziri hao walifuatia manaibu waziri ambao ni Mary Mwanjelwa (ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Costantine Kanyasu (Maliasili na Utalii), Innocent Bashungwa (Kilimo) na hatimaye Mwita Waitara (Tamisemi)
Mbali na mawaziri na manaibu pia ameapishwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha sheria Jaji Januari Msofe.
Leave a comment