February 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli avunja Bodi ya Ushauri TEMESA

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Pombe Magufuli ameivunja bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa inasema Rais Magufuli ameivunja bodi hiyo leo Jumapili tarehe 23 Septemba, 2018.

Bodi hiyo iliyokuwa inaongozwa na Mwenyekiti wake, Brigedia Generali mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri imevunjwa wakati Kamati maalum ya Uchunguzi wa ajali ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 20 ikianza kazi ya kuchunguza tukio hilo lililopoteza uhai wa watu zaidi ya 200.

error: Content is protected !!