Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Magufuli atunuku Kamishisheni Maafisa 146 wa JWTZ
Habari Mchanganyiko

Rais Magufuli atunuku Kamishisheni Maafisa 146 wa JWTZ

Dk. John Magufuli, Rais wa Tanzania
Spread the love

RAIS John Magufuli amewatunuku Kamisheni Maafisa wapya 146 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kundi la 65/18. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 30 Machi 2019 katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli wakati akizumnguza katika hafla hiyo, amewataka maafisa hao wapya wa JWTZ  kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria ili kuendelea kuimarisha uimara na sifa njema ya jeshi hilo.

Aidha, Rais Magufuli amelihakikisha jeshi hilo kwamba serikali iotaendelea kuliimarisha katika majukumu yake.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA), Brigedia Jenerali, Justice Mukande amesema maofisa waliotunukiwa Kamisheni leo walianza mafunzo tarehe 12 Machi 2018 wakiwa 236 ambapo 94 kati yao wameshindwa kufuzu kutokana na sababu mbalimbali.

Amesema  waliofuzu mafunzo hayo, wamefundishwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na kukubalika kimataifa.

Brig. Jen. Mukande amesema maafisa hao waliotunukiwa katika cheo cha Luteni Usu wana viwango mbalimbali vya elimu ambapo 3 wana Shahada ya Uzamili, 116 wana Shahada ya Kwanza na 3 wana Shahada ya Juu na 23 ni Madaktari wa binadamu.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!