October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa Kenyatta

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ametuma salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta kufuatia shambulizi la kigaidi lililopoteza maisha ya watu 21. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Tukio hilo ambalo linatajwa kutekelezwa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab, lilitokea katika hoteli ya DusitD2 iliyoko jijini Nairobi tarehe 15 Januari 2019, ambapo hadi sasa taarifa zinaeleza kuwa, watu 28 wamejeruhiwa huku wengine 19 wakipotea kusikojulikana.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Magufuli amempa pole Rais Kenyatta kwa kuandika kuwa, “Punde nimezungumza na Mhe. Kenyatta kuhusu shambulizi la Jijini Nairobi, zaidi ya watu 14 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa. Pole sana Mhe. Rais na pole sana wananchi wa Kenya. Tupo nanyi katika kipindi hiki cha majonzi. Nawaombea Marehemu wote walale mahali pema peponi, Amina.”

https://twitter.com/MagufuliJP/status/1085596624578056194

error: Content is protected !!