December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli atua Mtwara, mwili wa Mkapa wawasili Lupaso

Rais John Magufuli akiwasili Uwanja wa Ndege Mtwara

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara kwa ajili ya kushiriki shughuli ya mazishi ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Mwili wa Mkapa utazikwa kesho Jumatano tarehe 29 Julai 2020 nyumbani kwake kijijini Lupaso wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara.

Mkapa alifikwa na mauti Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa mshtuko wa moyo.

Tayari mwili wa Mkapa umekwisha kufika nyumbani kwake ambapo waombolezaji watapata fursa ya kuuaga.

Kiongozi huyo aliyezaliwa tarehe 12 Novemba 1938 aliongoza Tanzania kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

 

Mkapa ameacha mjane, Anna na watoto wawili wa kiume, Stephano na Nicolas.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!