July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli atoa wiki kwa wafanyabiashara kulipa kodi

Spread the love

RAIS John Magufuli ametoa siku saba kwa wafanyabiashara walioingiza mizigo yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria. Anaandika Erasto Masalu … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Ikulu, jijini Dar es Salaam na Rais Magufuli alipokutana na wadau wa sekta binafsi. Siku hizo sana zinaanzia leo Desemba 3, 2015.

Mkutano huo wa Rais Magufuli na wafanyabiashara hao ni sehemu ya kutumika ahadi yake ya kukuza uchumi kupitia kwa kupitia sekta binafsi, aliyoiahidi wakati wa kampeni zake.

Rais Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake amedhamiria kuijenga nchi na watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta maendeleo na siyo ujeuri.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amewaahidi wadau wasekta binafsi ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika kukuza uchumi na pia amewataka wadau hao kuwa wazalendo na kuliacha kukwepa kulipa kodi ili tuweze kujenga taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.

Rais Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa watakapokuwa tayari kuwekeza wafanye hivyo kama akikwamishwa na mtu aliyechini ya uteuzi wake basi mtu huyo ataondoka, kwani sasa ni wakati wa wadau wa sekta binafsi kuanza kuanzisha viwanda mbalimbali vitakavyotoa ajira.

Pia Rais Magufuli amewapa mawazo ya kibiashara wadau wa sekta binafsi kuanzisha kampuni ya kutenganisha udongo unaotoka kwenye machimbo ya madini, kuanzisha viwanda vya samaki pembezoni mwa bahari pamoja na kutengeneza samani zitokanazo na mazao ya misitu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Regnald Mengi amesema kuwa wako tayari kumpa ushirikiano mkubwa rais katika kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa kwa haraka.

Mengi pia amemuomba rais kuendelea kukemea masuala ya rushwa pamoja kusaidia kupunguza utitiri wa kodi.

error: Content is protected !!