Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli atia saini ujenzi wa daraja la Salender
Habari za Siasa

Rais Magufuli atia saini ujenzi wa daraja la Salender

Spread the love

RAIS John Magufuli amemtaka mkandarasi wa daraja la Salender kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa huku akiwataka kuwatumia wafanyakazi kutoka Tanzania. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Hayo amezungumza leo katika utiaji wa saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Selander lenye urefu wa kilomita 6.23 kutoka eneo la Coco Beach hadi Aga Khan unatarajiwa kufanyika kwa miezi 36.

Rais Magufuli amesema pamoja na mkataba wa ujenzi ni wa miezi 36 lakini anaomba ikiwezekana likamilike kabla ya muda huo ili adhma ya kupunguza foleni itimie mapema zaidi.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemtaka mkandarasi kuwatumia wafanyakazi kutoka Tanzania kwani nchini kuna watendaji kazi wa ngazi zote.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale amesema mradi huo umelenga kupunguza foleni jijini Dar es Salaam.

Utiaji saini ulishuhudiwa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-Yok aliye nchini kwa ziara ya kiserikali.

Mfugale amesema daraja hilo litagharimu Dolaza Marekani 126.26 milioni. Amesema Tanzania imechangia asilimia 17.2 na Korea Kusini asilimia 82.2.

Amesema daraja hilo litakuwa na uwezo wa kubeba tani 180 kwa wakati mmoja na magari 55,000 kwa siku moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!