April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ateua mwenyekiti mpya TASAC

Rais John Magufuli

Spread the love

MKUU wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Andrew Satta, ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC). Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, uteuzi wa Prof. Satta umeanza jana tarehe 23 Aprili 2019.

Vile vile, Rais Magufuli ameteua Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TASAC, akiwemo Daniel Mchome, Mussa Mandia, Evelyne Makala, Renatus Mkinga, Japhet Massele na Bernard Asubisye.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Emmanuel Ndomba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC.
“Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC na Mkurugenzi wa TASAC umeanza leo (jana) tarehe 23 Aprili 2019,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Msigwa.

error: Content is protected !!