
Rais John Magufuli
RAIS John Magufuli amemteua Dk. Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 25 Septemba 2019 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu.
Taarifa ya Msigwa inaeleza kuwa Dk. Msengwa ambaye ni Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anachukua nafasi ya Andrew Massawe, baada ya kumaliza muda wake.
“Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 19 Septemba 2019,” inaeleza taarifa ya Msigwa.
More Stories
Rais Mwinyi aukataa msamaha wa Mzee Shamte
Majaliwa ammwagia manoti aliyekuwa mraibu dawa za kulevya
Butiku ataka nguvu ielekezwe kwenye maendeleo ya wananchi kuliko vyama