September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi NHC

Spread the love

RAIS John Magufuli amemteua aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Dkt. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 30 Oktoba 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Katika hatua nyingine, taarifa hiyo inaeleza kuwa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi amemteua aliyekuwa Mhadhiri wa ARU, Dkt. Maulid Banyani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa.

“Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 30 Oktoba 2018,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

error: Content is protected !!