Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli ateua DC, Ma-DED 5
Habari za Siasa

Rais Magufuli ateua DC, Ma-DED 5

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya (DC) na Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) tano nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema uteuzi wa viongozi hao unaanza leo Jumanne tarehe 7 Julai 2020.

Msigwa amesema, Rais Magufuli amemteua Lauteri John Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Mkoa wa Njombe.

Kabla ya uteuzi huo, Kanoni alikuwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Songwe na anachukua nafasi ya Ally Mohammed Kasinge.

Pili, Rais Magufuli amemteua Bashir Paul Mhoja kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoa wa Iringa.

Kabla ya uteuzi huo, Mhoja alikuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoa wa Geita na anachukua nafasi ya Robert Mgendi Masunya.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Ramadhan Salmin Possi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani.

Kabla ya uteuzi huo, Possi alikuwa Afisa Mipango katika Jiji la Tanga Mkoa wa Tanga na anachukua nafasi ya Amina Kiwanuka ambaye amestaafu.

Nne, Rais Magufuli amemteua Baraka Michael Zikatimu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora.

Kabla ya uteuzi huo, Zikatimu alikuwa Afisa Mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mkoa wa Tanga na anachukua nafasi ya Margareth Jonathan Nakainga ambaye amestaafu.

Tano, Rais Magufuli amemteua John John Nchimbi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Nchimbi alikuwa Afisa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoa wa Morogoro.

Sita, Rais Magufuli amemteua Emmanuel Matinyi Johnson kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.

Kabla ya uteuzi huo, Emmanuel Matinyi Johnson alikuwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!