April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ateua bosi mpya MSD

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Dk. Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili tarehe 3, 2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema uteuzi wa Dk. Mhidize unaanza mara moja leo.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Brigedia Jenerali Mhidize anachukua nafasi ya Laurean Rugambwa Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Bwanakunu ameongoza MSD tangu tarehe 23, 2015 baada ya kuteuliwa na Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete tarehe 6,2015.

Kabla ya uteuzi huo, Bwanakunu alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ariel Glaser Paediatric AIDS Healthcare Initiative.

error: Content is protected !!