June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli atakiwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi

Spread the love

RAIS wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli ametakiwa kuendeleza juhudi zake za kupambana na wazembe kazini na hali hiyo isiwe nguvu ya soda. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo ametakiwa kuhakikisha anaboresha maslahi ya wataalamu nchini badala ya kuboresha maslahi ya wanasiasa jambo ambalo linasababisha utendaji kuwa mbovu huku wataaluma wengi wakikimbilia kwenye siasa na kuacha kazi zao za kitaaluma.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Habari, Ufundi na Utafiti (RAAWU), Kanda ya Kati na Katibu wa TUCTA Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online juu ya uanzaji wa utendaji wa kazi wa Rais Magufuli.

Mwendwa, amesema licha ya rais kufuta matumizi mbalimbali pamoja na safari za nje ni vyema akafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa maslahi ya watumishi hususani wataalam kama madaktari na walimu yanaboreshwa.

Mwendwa amesema anapingana na kitendo cha serikali kuboresha zaidi maslahi ya wanasiasa huku watumishi ambao ni wataalam wakiachwa pembeni bila kuboreshewa maslahi yao.

“Hii ni aibu sana kwa wabunge ambao wanafanya kazi kwa miaka mitano na wanalipwa kiinua mgogongo zaidi ya Sh. 200 milioni huku wafanyakazi ambao ni wataalam ambao wamelitumikia taifa zaidi kwa miaka 35 wanalipwa kiinua mgongo si zaidi ya Sh. 50 milioni.

“Si vibaya kujifunza kwa mataifa mengine ambayo yanafanya kila jitihada kuhakikisha wanaboresha maslahi ya wataalam ili kuwafanya watu hao kuachana na tamaa za kuingia katika siasa na kuachana na taaluma zao,” amesema Mwendwa.

Mwandwa alilazikika kutoa kauli hiyo kutokana na rais Magufuli kuonekana kupiga marufuku safari za viongozi huku akizuka katika wizarani mbalimbali kwa ajili ya kuangalia utendaji wa kazi.

error: Content is protected !!