Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli asema kulima mtoni ruksa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli asema kulima mtoni ruksa

Rais John Magufuli akiwa katika ziara yake mkoani Kagera
Spread the love

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Rais John Magufuli ameondoa amri ya kuwazuia wananchi kulima katika maeneo ya mito na kuwataka kuendelea kufanya hivyo hata kama maji yatasomba maza yao, anaandika Richard Makore.

Ametoa agizo hilo leo eneo la Kyaka mkoani Kagera katika ziara yake na kusema kwamba wananchi waachwe walime mahali popote hata kama ni kwenye mito.

Agizo hilo limekuja baada ya Rais Magufuli kusimamishwa na wananchi njiani huku mmoja wao akiibuka na kulalamika vijana kuzuiwa kulima na kufanya biashara katika maeneo yaliyo karibu na mito.

Mara kadhaa serikali kupitia kwa wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wamekuwa wakiwazuia wananchi kulima ama kufanya shughuli jirani na vyanzo vya maji ikiwamo mito kwa kuwa wanahataraisha kukausha maji.

TAARIFA KAMILI ANAGALIA VIDEO HII

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

error: Content is protected !!