April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli asamehe wafungwa 5,533

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 5,533 leo Desemba 9, 2019. Anaripoti Martin Kamote … (endelea)

Rais Magufuli ametoa msamah huo katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Muungano, yaliyofanyika jijiji Mwanza.

“Nilipotembelea Gereza la Butimba, niliumia sana kukuta wafungwa wengine kesi zao za kubambikiwa na najua hii iko nchi nzima, mwingine amefungwa kisa tu aligombana kidogo na Mpenzi wake au Mshikaji wake,” amesema Rais Magufuli.

Magufuli ameongeza kuwa; “Natangaza kuwasamehe wafungwa wengi leo wapatao 5,533 ni mara ya kwanza kwa msamaha mkubwa kama huu kutokea, najua watu watashangaa lakini nimeamua kutumia Siku hii ya Uhuru kusamehe maana sifurahi kuongoza nchi yenye watu wengi magerezani.”

Hata hivyo Magufuli amesema msamaha huu utawahusisha wafungwa waliofungwa kati ya kipindi cha siku moja hadi mwaka mmoja, na wale waliofungwa miaka mingi kama 30, 20 au 10 na wamebakiza muda mfupi kumaliza.

error: Content is protected !!