April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli asamehe wafungwa 3,530

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 26 Aprili 2019, ametoa msamaha kwa wafungwa 3, 530 pamoja na wenye maradhi mbalimbali. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Taarifa iliyoyolewa leo na Meja Jenerali Jacob Kingu, Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi imefafanua kwamba, miongoni mwa wenye maradhi ya Kifafa, Ukimwi, Kifua Kikuu na saratani wamejumuishwa kwenye msamaha huo.

Msamaha huo wa Rais Magufuli umetolewa leo ikiwa ni siku kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa hiyo imeeleza kwama, msamaha huo umetolewa na Rais Magufuli kwa kutumia madaraka aliyopewa katika Katiba ya Nchi, ibara ya 45 (1)(d).

Katika idadai hiyo ya waliosamehewa (3,530), jumla ya wafungwa 722 wataachiwa huru kutoka gerezani leo ambapo 2, 808 watabaki ili kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki kwa kuzingatia msamaha huo.

Pia, Rais Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa wote kupunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria ya magereza Sura ya 58.

Ufafanuzi wa punguzo hilo unaelekeza kwamba, wafungwa hao sharti wawe wametimiza robo ya adhabu zao gerezani isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika ibara ya 2 (1-xxi).

“Msamaha utawahusu wafungwa wagonjwa wa Ukimwi, Saratani, Kifua Kikuu ambao wapo kwenye hatua za mwisho za ugonjwa na wathibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa mkoa na wilaya,” imesema taarifa hiyo.

Rais Magufuli pia amewasamehe wafungwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70 kwenda mbele kwa sharti la umri huo kuthibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa na Wilaya.

Pia waliosamehewa ni wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

Wengine waliopata msamaa kutoka kwa Rais Magufuli ni wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili, lakini uthibitishwe na waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa na Wilaya na kwamba, wafungwa wenye adhabu ya kunyongwa ama kifungo cha maisha hawahusiki.

Wafungwa waliopatikana na makosa ya kujihusisha usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya kama cocaine, heroin, bangi na rusha hawatopata msamaha hupo.

“Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo pia hawatahusika,” imesema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

“Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au mlipuko isivyo kihalali nao pia hawamo”.

Wafungwa wengine ambao msamaha huo hauwahusu ni wanatumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka, kulawiti, ukatili dhidi ya watoto au kujaribu kutenda makosa hayo.

Pia waliohukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na za sekondari ambao walitenda kosa wakiwa na miaka 18 na kuendelea hawatahusika.

Rais hajawasamehe pia wafungwa wanaotumikia kifungo kwa amkosa ya wizi wa magari, pikipiki na uharibifu wa miundombinu.

Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao, utakatishaji fedha na uhujumu uchumi na waliowahi kupunguziwa kifungo na Rais ambao bado wanaendelea na kifungo kilichobakia.

Wafungwa wengine ambao hawatahusika na msamaha huo ni wale waliokatisha haki ya watoto kupata masomo, waliohusika kwenye utekaji watoto, ukatili dhidi yao, kupoka na kufanya biashara ya binadamu.

Imesema wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi, ubadhilifu wa fedha za Serikali na makosa ya kutoroka chini ya ulinzi halali au kusaidia kutendeka makosa hayo hawahusiki.

error: Content is protected !!