November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli arudi nyumbani Chato, afurahia maendeleo

Rais John Magufuli alipowasili nyumbani kwao Chato

Spread the love

RAIS John Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na maendeleo yaliyofikiwa na wananchi wa Wilaya ya Chato mkoani Geita. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza baada ya kuwasili wilayani humo leo tarehe 1 Julai 2019, Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Chato kwa maendeleo wanayopata kutokana na jitihada zao za utendaji kazi.

Rais Magufuli amewahimiza wananchi hao kuongeza juhudi na maarifa katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Nawapongeza sana wananchi wa Chato, mnachapa kazi kwelikweli na maendeleo yanaonekana, Chato inabadilika. Nilishasema asiyefanya kazi na asile, kwa hiyo tuendelee kushikamana kufanya kazi na kujenga nchi yetu,”amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewasili katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato, kwa ajili ya mapumziko.

error: Content is protected !!