March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli apokea hati ya mabalozi

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 4 Oktoba 2018 amepokea hati za utambulisho wa mabalozi watano watakaowakilisha nchi zao hapa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa mchana wa leo, inaeleza kuwa, hafla hiyo imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imewataja mabalozi hao akiwemo, Balozi mteule wa Ubelgiji hapa nchini Peter Van Acker, Balozi mteule wa Norway Elisabeth Jacobsen, na Balozi mteule wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg.

Wengine ni Balozi mteule wa Palestina hapa nchini Hamdi Abuali na Balozi wa Kuwait Mubarak Mohammad Alsehaijan.

error: Content is protected !!