January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli apewa somo

Spread the love

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa Tanzania inahitaji kufanya mabadiliko ya kimfumo kama inahitaji mabadiliko ya dhati. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Amesema hayo kwenye mahojiano maalum na kituo cha televisheni, kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) lazima kikubaliane na matwaka ya wananchi ya kutaka mabadiliko ya katiba.  

Amesema kuwa watanzania wasitarajie mabadiliko makubwa endapo kila mwaka wataendelea kukiweka madarakani CCM.

“Kuna watu wanajidanganya kuwa eti Rais Magufuli hana itikadi za kichama huko ni kujidanganya Magufuli ni kada wa CCM na ataendelea kuwa CCM,” amesema Prof. Kitila.

Amesema kuwa Rais wa awamu iliyopita mwanzoni alionekana kuwa na utashi wa kuwaletea Watanzania katiba mpya lakini mwishowe alizidiwa na nguvu ya chama chake.

error: Content is protected !!