August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli apangua baraza la Mawaziri

Mwigulu Nchemba

Spread the love

DK John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya maabdiliko ya baraza la Mawaziri wake kwa kumteua Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, anaandika Hamisi Mguta.

Mwigulu Nchemba aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo sasa ametuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi. 

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu.

Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Charles Kitwanga, aliyekua waziri wa wizara hiyo ambaye alitenguliwa nafasi hiyo kutokana na tuhuma za kuingia Bungeni akiwa amelewa na kushindwa kujibu maswali.

Dk. Charles Tizeba, ni Mbunge wa Buchosha kuwa ambaye amewahi kuwa naibu Waziri wa Wizara ya uchukuzi wakati wa uongozi wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Mawaziri hao wote wawili wataapishwa 13 Juni mwaka huu, Ikulu.

error: Content is protected !!