September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli aongeza siku 20 usajili wa laini

Rais John Magufuli akisajili laini yake kwa alama ya vidole

Spread the love

RAIS John Magufuli ameongeza siku siku 20 kwa usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole kama ilivyotangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na baada hapo laini zote zitazimwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea). 

Hapo awali TCRA ilitangaza siku ya mwisho ya kusajili laini zote kwa alama za vidole kuwa ni tarehe 31 Desemba, 2019 ambapo zilikuwa zimebaki siku nne kabla ya kufikia mwisho.

Rais Magufuli ametangaza ongezeko hilo la siku 20 baada ya kusajili laini yake kwa njia ya alama za vidole leo akiwa mapumzikoni Chato.

Ongezeko hilo la muda litaanzia tarehe 1 Januari, 2020 na kufikia kikomo tarehe 20 Januari, 2020 ambapo amesema baada ya hapo ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha nyongeza laini zao zitazimwa.

error: Content is protected !!