June 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Rais Magufuli anajenga upinzani’

Spread the love

HATUA ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya imetajwa kuathiri zaidi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuliko vyama vya upinzani, anaandika Pendo Omary.

Wakizungumza na MwanaHALISI Online leo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamesema, hatua hiyo inachangia kuwajenga wabunge wa upinzani ambao sasa taarifa zao zinafika zaidi kwa wananchi kuliko za wabunge wa CCM.

“Ni wazi serikali na CCM wanashirikiana kudhibiti bunge lisirushwe ‘live’ wakiwa na lengo la kuwakomoa wapinzani. Wabunge wa CCM nao wanafurahia hatua hii.

“Wananshidwa kujua wao wenyewe wanajinyimwa fursa wananchi kuona mambo mazuri yanayosemwa bungeni na mawaziri wao,” amesema Khamis Rajabu, Mkazi Kariakoo.

Grace Lameck, Mkazi wa Mwananyamala amesema, “Sasa tunaelewa kwa nini bunge linazuiwa kurushwa ‘live’, ni kuficha udhaifu wa wabunge wa CCM.

“Mfano ni hili sakata la Goodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga (CCM) hivi karibuni kudai kwamba, anayeteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lazima aitwe ‘beby’ ikiwa na maana ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi. Huku ni kufilisika hoja,” amesema Grace.

Grace amesema tarehe 13 Mai, 2016 baada ya Nape Nnauye ambaye ni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 Mlinga alisema “ingekuwa amri yangu tungechonga sanamu la Diamond tukaliweka kwenye mnara wa Askari, ule mnara tumeuchoka.”

Na kwamba, kauli hiyo imechangia wanachi kukosa imani na uteteuzi wa wabunge wa CCM kuhusu kutorushwa bunge moja kwa moja.

Akiandika katika ukurasa wake wa Facebook, Irene Kiria, Mkazi wa Dar es Salaam anasema “bado sijaelewa kwa nini Bunge limeamua kuwapa upinzani umaarufu kiasi hiki. Social media (mitandao ya kijamii) imetaja zaidi yanayosemwa au kufanywa na wabunge wa upinzani kuliko wa CCM lakini mabaya ya CCM kuliko ya wapinzani.

“Kwa utendaji wa Rais Magufuli ulivyokubalika, wengi wetu tulipata mashaka iwapo upinzani utakuwa na nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano. Binafsi nikiri sasa kwamba, nilikuwa miongoni mwa waliojiuliza hivyo, kumbe nilikosea,” ameandika Kiria.

Pia Kiria ameanndika “kuzuia bunge ‘live’ ni ushahidi kwamba kimwili tunaishi katika karne ya leo lakini fikra na matendo yetu bado yako karne iliyopita. Matokeo ni huu mkanganyiko tunaoshuhudia, kulifanya jambo kusambaa na kufahamika zaidi kwa kitendo cha kujaribu kulizuia.

“Nadhani serikali na CCM wanatakiwa kutathmini namna wanavyoathirika kwa kufuta bunge ‘live’ isipokuwa kama hilo ndilo lengo lenyewe – kuwafanya wapinzani wang’are zaidi.”

 

error: Content is protected !!