Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli amwokoa Sugu
Habari za Siasa

Rais Magufuli amwokoa Sugu

Spread the love

RAIS John Magufuli ameagiza Hoteli ya Desderia inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, isivunjwe. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi tarehe 26 Desemba 2020 na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alipotembelea hoteli hiyo.

Chalamila amssema Rais Magufuli ameagiza hoteli hiyo isibomolewe kwa kuwa ujenzi wake ulifuata sheria.

“Rais Magufuli amenituma nije nikueleze (Sugu), kwamba hakuna mtu yeyote kuja kugusa na kusema anabomoa hoteli hii, sababu huyu ni muwekezaji kama wengine,” amesema Chalamila.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya, amesema Rais Magufuli ameagiza Sugu apewe viwanja katika mkoa huo, kama anataka kuwekeza.

Aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu

“Na amesema kama kuna viwanja vingine Uzunguni, anayestahili kunufaika navyo akiwemo Sugu apewe,” amesema Chalamila.

Chalamila amesema taarifa zilizoibuka hivi karibuni, kwamba hoteli hiyo inatakiwa kubomolewa kutokana na ujenzi wake kukiuka sheria kwa kujengwa katika vyanzo vya maji, si za kweli.

Amesema ujenzi huo ulifuata sheria kwa kuwa ardhi yake ilipimwa kisha hati yake kutolewa na mamlaka husika.

“Ardhi hii imepeimwa na ina hati, mkurugenzi wa ramani analifahamu hili eneo, kama vibali vyote vimefuata mlolongo wake, anatunza maji yake vizuri hayajakauka,” amesema Chalamila.

Kwa upande wake Sugu, amemshukuru Rais Magufuli kwa agizo hilo, na kusema kwamba hatua hiyo itawapa imani watu kuja kuwekeza nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!