RAIS John Magufuli ameagiza zitolewa Shilingi bilioni tisa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Jiji la Mwanza, anaandika Moses Mseti.
Ametoa agizo hilo leo alipofungua daraja la wapita kwa miguu la Furahisha lililpo jijini Mwanza na kusema kuwa mradi huo ni muhimu kwa wakazi wa Mwanza.
Akizungumzia ujenzi wa uwanja huo, Rais Magufuli amesema utasaidia kuinua uchumi kwa kuwa malengo ya serikali na kutaka kuona ndege kubwa zinatua katika eneo hilo katika miaka ijayo.
Aidha, aliwaambia wakazi wa Mwanza kwamba ujenzi wa Meli mpya ya kisasa itakayokuwa ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba unatarajia kuanza mapema mwaka ujao.
Miradi mingine ambayo itazinduliwa na Rais Magufuli mkoani Mwanza ni pamoja na viwanda.
Leave a comment