June 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ammwaga Anne Kilango

Spread the love

RAIS John Magufuli amemfuta kazi Anne Kilango Malecela, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Abdul Dachi, Katibu Tawala wa mkoa huo kwa kusema uongo, anaandika Faki Sosi.

Rais Magufuli amewafuta kazi watumishi hao leo wakati akipokea hundi ya Sh. 6 bilioni zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati.

Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na uongo huo, hivyo ameagiza Kilango, Dachi kuondolewa ofisini mara moja.

Kilango na Dachi walidanyanya kwamba mkoa huo hauna watumushi hewa ambapo baada ya uchunguzi kufanyika imebainika kuwepo na watumishi hewa 45.

Kilango alikuwa Mbunge wa Same Mashariki (2010-2015), aligombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana aliangushwa na Naghenjwa Kaboyoka wa Chadema.

Rais Magufuli alimteua Kilango kuwa Mkuu wa Mkoa wa Sinyanga tarehe 13 Machi mwaka huu.

Kilango anakuwa mkuu wa mkoa wa kwanza katika utawala wa Rais Magufuli kuachishwa kazi kutokana na uongo.

error: Content is protected !!