March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli amuapisha Dk. Ndumbalo huku akimuhurumia

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema anamuonea huruma Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, kwa kuwa anakwenda kufanya kazi ngumu iliyomshinda mtangulizi wake na kupelekea uteuzi wake kutenguliwa, Dk. Susan Kolimba. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Rais Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 29 Septemba 2018, baada ya kumuapisha Dk. Ndumbaro Ikulu jijini Dar es Salaam, huku akieleza baadhi ya sababu za kutengua uteuzi wa Dk. Kolimba na kumhamisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda ambaye amemteuwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Kuna mikutano mingi Waziri atakuwa anatumwa na hata wewe, waziri muda mwingi anakuwa nje ya Tanzania ndiyo maana kuna naibu waziri, waziri akiwa hayupo naibu anakuwa msimamizi wa mambo yote, siyo naibu waziri kuendeshwa na wakurugenzi, na ndio maana nikaona nimtoe naibu waziri na katibu mkuu, nazungumza kwa uwazi bila kuficha,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.

“Inawezekana ukafurahi kuteuliwa lakini nakuonea huruma sababu unakwenda kufanya kazi ngumu, wizara ya mambo ya nje mambo hayaendi vizuri, inawezekana wakurugenzi wako weak (dhaifu)sana au wamezoea ‘business as usually’. Ikitokea ukienda huko usipoangalia nikikutumbua usije kulaumu.”

Dk. Magufuli amesema baadhi ya watendaji hasa wakurugenzi wa Wizara hiyo wanafanya kazi kwa mazoea, ambapo amemuagiza endapo atabaini kuna mtendaji au mkurugenzi mzigo ashaurinane na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine mahiga ili waondolewe kazini.

“Nataka ukafanye kazi wakajue Ndumbaro yupo, kama kuna maeneo yanatakiwa yafanyiwe marekebisho ufanye, kama kuna wakurugenzi ni mizigo kashauriane na waziri wako watoke, wapo watu wanahisi watakaa foreign ‘mambo ya nje’ hadi wastaafu,” amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!