RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua, Dk. Godwin Mollel kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea)
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi tarehe 16 Mei, 2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, uteuzi wa Dk. Mollel ambaye ni Mbunge wa Siha (CCM) unaanza leo.
Dk. Mollel anachukua nafasi ya Dk. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni kupitia CCM ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Dk. Ndugulile amekuwa naibu waziri wa wizara hiyo tangu tarehe 9 Oktoba, 2017 alipoapishwa na Rais Magufuli akichukua nafasi ya Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye alipandishwa na kuwa waziri wa maliasili na utalii.
Leave a comment