Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli amtumbua DED
Habari za Siasa

Rais Magufuli amtumbua DED

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Revocatus Kuuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora  … (endelea).

Ametengua uteuzi kufuatia tuhuma za kujitwalia ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na ubadhilifu wa fedha za maduhuli ya Serikali zinazomkabili Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu tarehe 28 Desemba 2020, aliposimama kuwasalimu wananchi wa Igunga wakati akiwa safarini, ambapo wananchi na viongozi wa Tabora wamepata fursa ya kueleza kero zao.

Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dk. Phillemon Sengati kuteua mtumishi mwadilifu atakayekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mpaka hapo uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji mwingine atakayeendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano utakapofanyika.

Rais Magufuli amesema pamoja na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, anazo taarifa nyingi za dosari za Kuuli, alishamuonya juu ya vitendo vyake vya kuwadhulumu wananchi wakiwemo wanawake na hivyo Serikali anayoiongoza haiwezi kumvumilia kiongozi wa namna hiyo.

“Suala la mkurugenzi wa hapa ninalifahamu, nina ripoti nyingi zinazomhusu yeye. Kuna wakati nilimtuma mkuu wa mkoa kuja kushughulikia issue (suala) yake. Kwa sababu ya haya bado hajajirekebisha, nina msimamisha kazi kuanzia leo.  Huko aliko ajue kwamba hana kazi ya kuwa mkurugenzi wa hapa Igunga,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Tabora Dk. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja.

“Kwa hiyo, mkuu wa mkoa na uongozi wa Igunga makae,  mteua mtu ambaye ana nidhamu, hatadhurumu watu. Aanze kukaimu wakati napanga mipango ya kuteua mkurugenzi mwingine wa kuja hapa atakaye enda na kasi yangu,” amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewashukuru wananchi wa Igunga na Watanzania kwa ujumla kwa kumchagua kwa kura nyingi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili na ameahidi kuwatumikia kwa uwezo wake wote.

Amewapongeza wananchi wa Tabora, Igunga na Nzega kwa kupata maji kutoka Ziwa Victoria na amewasihi kutumia maji hayo vizuri kwa manufaa yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!