June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli apitisha fagio RAHCO, TRL

Spread the love

RAIS John Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hodhi ya Rasilimali ya Reli Tanzania (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatiwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika kuwa mchakato wa utoaji wa zabuni za ujenzi wa reli.

Akitoa kauli hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli amefikia hatua hiyo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu wa wizara na taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani ‘Standard Gauge.’

Balozi Sefue amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mhandisi Tito, pia Rais Magufuli amevunja bodi ya RAHCObaada ya kujiridhisha kuwa haikutelekeza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala yake walikuwa wanatetea kilichofanyika.

Aidha Rais Magufuli amemtaka Mhandisi Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi wa zabuni hiyo.

Pia Rais Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) uchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo zitathibitika kama zimeshiriki ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amevunja Bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa jinsi ya bodi hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mvchakato wa manunuzi hya mabehewa ya treni.

error: Content is protected !!