April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli amteua Dk Mwigulu kumriti Balozi Mahiga

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dk. Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa katiba na sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …. (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi tarehe 2, 2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema uteuzi wa Dk. Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi kupitia CCM umeamza leo.

Msigwa amesema Dk. Mwigulu anachukua nafasi ya Balozi Augustine Mahiga aliyefariki dunia jana Ijumaa tarehe 1 Mei, 2020.

Mwili wa Balozi Mahiga umezikwa leo Jumamosi kijijini kwao Tosamaganga mkoani Iringa ambapo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliwaongoza waombolezaji kuhitimisha safari ya mwisho hapa duniani ya mwanadiplomasia huyo mashuhuri.

Dk. Mwigulu anarejea tena ndani ya baraza la mawaziri baada ya tarehe 1 Julai 2018 Rais Magufuli kutengua uwaziri wake wa mambo ya ndani kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa sababu ambazo Rais Magufuli alizieleza za kutengua uteuzi wake ni Dk Mwigulu kushindwa kushughulikia azimio la Bunge kuhusu kushughulikia suala la kufunga mashine za alama za kielektroniki za utambuzi wa alama za vidole (AFIS) katika vituo 108 vya polisi uliofanywa na kampuni ya Lugumi kwa gharama ya bilioni 37.

Nyingine ni mkataba wa ununuzi wa magari 777 ya polisi, kushughulikia changamoto zinazolikabili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ajali barabarani, usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO), kupandishwa vyeo kwa askari, masuala ya wakimbizi na kuhakikisha wafungwa wanazalisha mali.

error: Content is protected !!