Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli amsifu Jakaya Kikwete
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli amsifu Jakaya Kikwete

Spread the love

RAIS John Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete kwa kuanzisha ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ujenzi wa jengo hilo uliogharimu kiasi cha Sh. 788.6 Bilioni, ulianza mwaka 2013 ambapo leo tarehe 1 Agosti 2019 Rais Magufuli alilizindua kwa ajili ya matumizi.

Akikziungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Rais Magufuli amempongeza Dk. Kikwete kwa hatua hiyo, akisema kwamba jengo hilo litaongeza kasi ya kuhudumia abiria wanaosafiri kwa ndege.

“Nichukue nafasi hii kwa dhati kabisa kumshukuru Mheshimiwa Jakaya Kikwete ambaye ni mwanzilishi wa hili, mimi nimekuja kukamilisha,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, jengo hilo litaongeza uwezo wa JNIA kuhudumia abiria kutoka Milioni 2 hadi Milioni 8 kwa mwaka.

“Nimearifiwa kuwa uwezo wa jengo la kwanza Terminal 1 ni abiria laki 5 kwa mwaka, la pili ni milioni 1.5 na la leo lina uwezo wa  mil 6 kwa mwaka. Hivyo kiwanja kitahudumia abiria milioni 8 nane kwa mwaka. jengo hili litaongeza kasi ya kuhudumia abiria wanaosafri kwa ndege,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ameipongeza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kwa kusimamia vyema ujenzi wa jengo hilo baada ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kusua sua kutekeleza mradi huo.

“Wakati tunaingia madarakani mradi huu ulisimama na ukakosa pesa na mkandarasi alikuwa anatudai fidia ya kutofanya kazi. Tunashukuru tuliweza kutafuta fedha kwa haraka ili mradi ufanyike na sasa umefanyika, “amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Niseme kwa uwazi TAA walishindwa kuusimamaia mradi huu, na ndio maana tukaamua viwanja vya ndege vyote nchini  sasa viwe vinasimamiwa na Tanroads kama ilivyokuwa zamani. Tunashukuru kazi mmeifanya, Mfugale na watu wako mmefanya kazi kubwa sana.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!