Spread the love
UTEUZI wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Dk. James Wanyancha umetenguliwa, anaandika Pendo Omary.
Hatua hiyo imechukuliwa na Rais John Magufuli mapema hii leo huku sababu za kutenguliwa kwa uteuzi huo zikiwa hazijawekwa wazi na mamlaka ya uteuzi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo mjini Dodoma imesema, “kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Joseph Odo Haule kuwa mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.”
Hata hivyo wajumbe wengine wa bodi ya mfuko huo wametakiwa kuendelea na nafasi zao kama kawaida.
Kabla ya uteuzi huo, Haule alikuwa meneja wa mfuko wa barabara.
More Stories
Mrithi wa Maalim Seif, siri nzito
Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco
Rais Magufuli amuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya