Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli akata ngebe za wanaoibeza Dreamliner
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli akata ngebe za wanaoibeza Dreamliner

Spread the love
RAIS John Magufuli amekata mzizi wa fitina kwa wanaoibeza ndege ya Dreamliner wakidai mbovu, baada ya kuamua kutumia ndege hiyo kwenda jijini Mwanza leo Jumamosi tarehe 18 Agosti, 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Katika safari hiyo Rais Magufuli alitumia kuzungumza na abiria waliopanda ndege hiyo ikiwa pamoja na kupiga nao picha mbalimbali kama kumbukumbu.

Ndege hiyo ilizua gumzo mitandaoni wiki iliyopita baada ya kusimamisha huduma kwa matengenezo ya kawaida kabla ya kuanza tena safari zake za kawaida za Dar es Salaam, Moshi na Mwanza.

Kitendo cha Rais Magufuli kutumia ndege hiyo kubwa zaidi nchini, ni kuwahakikishia wananchi kuwa ipo salama na wamezungumza na kuwapongeza wananchi waliosafiri nao pamoja.

Rais Magufuli baada ya kushuka uwanja wa Ndege wa Mwanza alikwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akapopokewa na viongozi kadhaa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Wakati akitoka katika hospitali hiyo alisimamisha msafara wake na kuzungumza na wanafunzi wa Shule Msingi Mongella iliyopo eneo la Bugando waliokuwa wamesimama pembeni mwa barabara.

“Mmekuja kufanya nini hapa,” Rais Magufuli aliwauliza swali wanafunzi hao. Kwa sauti ya pamoja, wanafunzi hao wakajibu “Tumekuja kukuona”

Baada ya jibu hilo, Rais Magufuli aliwashukuru wanafunzi hao na kuwaambia, “Nitarudi siku nyingine kuonana na kuzungumza nanyi. Leo nimefika hapa kumuona mgonjwa wangu ambaye amelazwa hapa hospitalini. Endeleeni kuwaombea wagonjwa waliolazwa hospitalini.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!