July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ‘aichoka’ TPSF

Spread the love

RAIS John Magufuli ameonesha kutofurahishwa na utendaji kazi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), na kushauri kwamba, kama imeshindwa kutatua changamoto za wafanyabaishara, kianzishwe chombo kingine. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wake na wafanyabaishara zaidi ya 1,000 kutoka mikoa yote Rais Magufuli amhoji kwamba, je kuna sababu ya kuanzisha chombo kingine ambacho kitakuwa kiunganishi cha wafanyabiashara kwenye maeneo yao?

Rais Magufuli amehoji hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabaishara kwamba, TPSF imekuwa jukwaa la kuwagandamiza wafanyabiashara wengi na kutengeneza kundi wanalolitaka wao.

“Wapo wengine na hili nataka nizungumze Bwana Shamte (Salum Shamte, Mwenyekiti TPSF) baadhi ya wafanyabaishara wamekuwa wakizungumza, inawezekana leo wakaogopa kuzungumza hapa wewe upo, wanasema TPSF imekuwa jukwaa la kuwagandamiza wafanyabaishara.

“…na kutengeneza ‘group’ (kundi) la watu fulani fulani wanaojiita wawakilishi wa wafanyabaishara mtayajibu ninyi wenyewe, mimi jukumu langu ni kusema,  je kuna sababu ya kuanzisha chombo kingine ambacho kitakuwa ‘direct link’ na watu wengine katika maeneo yao?”

Mbele ya Shamte,  Rais Magufuli amesema, yeye sio mnafiki na kwamba, panapohitajika kueleza ukweli, atafanya hivyo ili wahusika wajirekebishe.

 “Ukiwa msemaji wa wafanyabiashara lazima ujue biashara inaendeshwaje, najaribu kuyazungumza haya wenzangu mimi sio mnafiki. Mimi napasuaga hapo hapo, huku unaniangalia huku nalisema hivyo hivyo.

“Ili kusudi tufike mahali tujirekebishe,  ‘ku-formulate’ (kufanya) kitu ambacho kitawasemea ninyi wafanyabaishara,” amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!