Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli agusa maisha ya Rugemarila, Seth
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli agusa maisha ya Rugemarila, Seth

Spread the love

RAIS John Magufuli ameshauri wafungwa walioko mahabusu kwa tuhuma za uhujumu uchumi, kama wako tayari kuomba radhi na kuzirudisha fedha walizotafuna, watolewe. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Miongoni mwa wafungwa waliopo mahabusu kwa tuhuma hizo ni pamoja na wafanyabiashara wakubwa nchini Harbinder Seth na James Rugemalira.

Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwemo kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22 milioni.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2013 ambapo walikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza mwaka 2017.

Rais Magufuli ameshauri hayo leo tarehe 22 Septemba 2019, wakati anawaapisha viongozi mbalimbali aliowateuwa hivi karibuni, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli amemshauri  Biswalo Mganga, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DPP) kama sheria inaruhusu, awasikilize watuhumiwa watakaokuwa tayari kuomba msamaha na kuzirejesha fedha hizo.

“Wapo watu wamekaa mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi,inawezekana wapo tayari kuomba msamaha na kurejesha pesa, DPP katika kipindi cha siku saba ningeshauri kama sheria inaruhusu wakatoke humo ndani, haya nimapendekezo sijaingilia mahakama,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!