July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli afuta sherehe za 9 Desemba

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amesitisha sherehe za maadhimisho ya Uhuru za mwaka huu na ameagiza siku hiyo itatumiwa kwa kusafisha mazingira kutokana na nchi kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali, Barozi Ombeni Sefue amesema kuwa sherehe hizo zinazofanyika kila mwaka Desemba 9, kuwa haitakuwa yenye shamlashamla za zinazoifanya serikali kutumia fedha nyingi na baadala yake kutumia siku hiyo kwa taifa zima kwa kusafisha mazingira ili kuondokana na vimerea vya ugonjwa huo.

Balozi Sefue amesema fedha ambazo zitatumika katika sherehe hizo ziwekwe kwenye mipango mingine ya kiserikali pamoja na siku hiyo kutafanyika usafi wa mazingira nchi nzima.

Amesema kuwa maadhimisho hayo yanaigharimu serikali kiasi cha fedha ambacho hakuwa tayari kuweka wazi na kusitisha kwa sherehe hizo kutokuwa kiasi hicho.

Balozi Sefue ameagiza kwa viongozi mbalimbali wa halmashauri, miji na majiji kuhakisha kuwa watu kwenye mamlaka zao wanashirirki kwenye zoezi hilo.

Sherehe hizo zinazofanyika kila mwaka Desemba 9 kutokana na siku hiyo nchi ya Tanzania ilitwaa Uhuru wake kutoka mikononi mwa wakoloni wa kiengereza.

error: Content is protected !!