Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli afunga mjadala kuhusu katiba mpya
Habari za Siasa

Rais Magufuli afunga mjadala kuhusu katiba mpya

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amefunga mjadala kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, akisema kuwa hategemei kutenga fedha kwa ajili ya mchakato huo kwa sasa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumza katika kongamano kuhusu hali ya uchumi na siasa nchini lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuliko fedha kutumika katika mchakato huo, ni bora zielekezwe katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli.

Aidha, amesema kama kuna watu wanataka kusaidia kutoa fedha kwa ajili ya mchakato huo, ni bora wasaidie katika ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge-SDG).

“Tusitumie hela ya kupeleka watu bungeni wakalipane posho za kila siku, tunataka hizo fedha zitumike kujenga reli, SDG, kuimarika kilimo, na ndio maana kuna mataifa makubwa katiba zao zimeundwa miaka kadhaa zilizopita. Tutakaa kubishana kupoteza pesa ‘for nothing’, huu si wakati wake,”amesema na kuongeza Rais Magufuli.

“Sitegemei kupanga hela kwa ajili ya watu kula kwa sasa hivi, na kama wako watu wanataka kutusaidia hizo fedha, watusaidie kujenga reli na SDG. lakini sikatai kusikiliza maoni ya watu, kuna ushauri tunapokea, Lakini ninachotaka kuwambia tunaenda vizuri.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!