RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amefariki dunia jana Jumatano, tarehe 17 Machi 2021, saa 12:00, katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam, kwa maradhi ya moyo. Anaripoti Mwandishi Wetu.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akitangaza msiba huo mzito kwa Taifa, amesema, Rais Magufuli alianza kuumwa tatizo la mfumo wa umeme wa moyo tarehe 6 Machi 2021 na kutibiwa Hospital ya Moyo ya Jakaya Kikwete kisha kuruhusiwa 7 Machi 2021, kuendelea na majukumu yake.
Mama Samia amesema, tarehe 14 Machi 2021, hali yake ilibadilika na kupelekwa Hospital ya Mzena, Dar es Salaam hadi mauti yalipomfika.
Makamu huyo wa Rais, ametangaza siku 14 za maombolezo na bendera zitapepea nusu mlingoni huku taratibu zingine za mazishi zikiendelea.
Dk. John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 huko wilayani Chato Mkoani Kagera (hivi sasa Chato ni wilaya ya mkoa mpya wa Geita).
Aliingia madarakani kama Rais kwa mara ya kwanza tarehe 5 Novemba 2015, akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekua amemaliza muda wake wa utawala wa miaka kumi.
Dk. Magufuli, alifanikiwa kutetea nafasi hiyo tena katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana-2020 na kuapishwa tarehe 5 Novemba 2020, ili kuhitimisha miaka kumi ya utawala wake.
kiukweli hakuna anayeamini asee
ningumu kuamini nila INA LILLAH WAINA ILLAIH RAJIUN
Mungu wetu wa Mbinguni, ni vigumu mno kuamini taarifa hizi. Tunaomba umpe mapunxiko ya Amani baba yetu JPM. “Amin”
R.I P ndgu yetu
R I P
Tunakuomba mola wetu umsamehe yote aliyokukosea