April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli afanya uteuzi wa RAS, DC

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dk. Delphine Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (RAS). Aanaripoti Mwandshi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Magere anachukua nafasi ya Theresia Mmbando ambaye amestaafu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 6, 2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema kabla ya uteuzi huo, Dk. Magere alikuwa Ofisi ya Rais akishughulikia masuala ya uchumi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dunstan Kyobya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara (DC), mkoani Mtwara.

Kyobya anachukua nafasi ya Evod Mmanda aliyefariki Dunia tarehe 27 Aprili, 2020.

Kabla ya uteuzi huo, Kyobya alikuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 06 Mei, 2020.

error: Content is protected !!