April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli afanya uteuzi, atengua

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 19 Oktoba 2019 amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Rais Magufuli amemteua Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Kabunduguru aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia elimu, anachukua nafasi ya Hussein Katanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Pia, Rais Magufuli amemteua Godfrey Mweli, kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia elimu. Kabla ya uteuzi huo, Mweli alikuwa Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Hashim Komba, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea akichukua nafasi ya Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Hali kadhalika, Rais Magufuli amemteua Hassan Rungwa, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.

error: Content is protected !!