Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli aeleza kilichokwaza malipo zao la korosho
Habari za Siasa

Rais Magufuli aeleza kilichokwaza malipo zao la korosho

Dk. John Magufuli, Rais wa Tanzania
Spread the love

KUWEPO kwa majina hewa takribani 780, kumetajwa kuwa miongoni mwa sababu za serikali kuchelewa kulipa wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hayo amesema Rais John Magufuli leo tarehe 2 Aprili 2019 mkoani Mtwara, wakati akielezea changamoto zilizochelewesha baadhi ya wakulima wa korosho katika maeneo mbalimbali kulipwa fedha zao.

Rais Magufuli ameeleza kuwa, uhakiki uliofanywa na serikali katika orodha ya majina ya wakulima wa korosho, ulibaini kwamba kuna majina ya watu 780 ambao taarifa zao hazikuonesha kama wana mashamba ya korosho.

“Tukasema tufanye uhakiki, maana Watanzania ni mabingwa kwa hewa, nilipoingia madarakani nikakuta watumishi hewa. Tulipofanya uhakiki, majina ya watu 780 yaliorodheshwa ambao hawana shamba wala mikorosho, lakini wanadai wana kilo 1,500,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema miongoni mwa watu waliokom katika majina hayo, huenda wakawa watu walionunua korosho zilizokuwa mashambani wanaofahamika kama ‘Kangomba’

Akizungumzia kuhusu changamoto zilizochelewesha baadhi ya wakulima kuchelewa kulipwa fedha zao, amesema tofauti katika utoaji wa taarifa za wakulima wa korosho ni miongoni mwa sababu zilizochelewesha malipo hayo.

“Wako wengi  hawajalipwa kwa sababu nyingi tu, wapo waliowekewa fedha benki unakuta akaunti aliyotaja jina ni tofauti na lake, wapo waliokuwa hawana akaunti wakazungumza nenda kalipie kwenye akaunti ya shangazi, sasa hela ya serikali haiendei hivyo, ukishataja akaunti yako lazima fedha iende kwenye akaunti yako,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameagiza viongozi wa mkoa na Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua watu wanaoandika majina hewa kwa kuwa wanachelewesha zoezi la serikali la kulipa wakulima wa korosho.

“MaRPC muwashughulikie watu wanaoandika majina ambayo hayapo, wanatucheleweshea tunataka tushughulikie ili tujiandae na msimu unaokuja. Nitoe wito kwa vyama vya ushirikia mkoa huu wabadilike tabia yao ya kufanya biashara kwa wakulima wanyonge, “ amesema Rais Magufuli.

Aidha, amewaonya watu wanaotoa taarifa za uongo ya kwamba serikali haijawalipa fedha zao, na kuagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua mapema wanapobainika ikiwemo kuwaweka ndani.

“Wapo watu wa namna hii ambao wamelipwa hela wamezitumia vibaya wanalalamika korosho, wako  wanaume kama mimi ana wake wawili watatu maana inaruhusiwa, hela anapata anapeleka nyumba ndogo halafu kwingine anasema korosho sijalipwa sasa mzizi wa fitina uko hapa, kawaumbue wote wanaosema hawajalipwa, na wanaosema hawajalipwa wakati orodha yake iko humu mshike muweke ndani,” ameagiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewahakikishia wkaulima kwamba serikali yake itaimarisha uchumi wa wakulima kwa kuhakikisha hawalaliwi na wafanyabiashara wanapouza mazao yao.

“Serikali yangu tunataka kuimarisha kiuchumi wanufaike na majasho yao, uamauzi wa kununua korosho sio kwamba inataka kufanya biashara, ni kawaida ya serikali makini kusaidia wananchi wake. Haya yamekuwa yakifanyika, “ amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!