Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli aeleza corona ilivyo fursa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli aeleza corona ilivyo fursa

Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania, kulima mazao hasa ya chakula, ili kuzisaidia nchi ambazo zinashindwa kulima kutokana na kufungiwa ndani, kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato…(endelea).

Amesema hayo leo tarehe 17 Januari 2021, wakati akitoa salamu zake baada ya kuangana na waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria, Parokia ya Chato Mkoani Geita kusali Misa Takatifu (Dominika ya 2 ya Mwaka B) iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padre Henry Mulinganisa.

Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amewapongeza waumini wa Kanisa hilo kwa kufanikisha upanuzi wa Kanisa lao ambalo sasa lina nafasi ya kutosha Waumini wengi zaidi kufanya Ibada kwa wakati mmoja.

Rais Magufuli ametoa wito kwa waumini hao na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake kwa Taifa na hasa kwa kuepusha janga la ugonjwa wa Corona (Covid -19), nchini Tanzaniailihali ugonjwa huo ukiendelea kusababisha vifo vya maelefu ya watu katika nchi nyingine duniani.

Amesisitiza kutokana na Tanzania kuepushwa na ugonjwa huo, Watanzania wanapaswa kutumia nafasi hii kuchapa kazi zaidi hasa kuzalisha mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya chakula kwa ajili ya kuzisaidia nchi ambazo zinashindwa kufanya uzalishaji kutokana na watu wake kufungiwa majumbani (lockdown) na pia kukuza uchumi.

“Sasa hivi mvua zinanyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, nawaombeni sana ndugu zangu Watanzania tulime mazao hasa ya chakula, tulime kwa wingi ili baadaye tuje kuwasaidia wenzetu ambao wanashindwa kulima kutokana na Corona” amesema Rais Magufuli.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Alichokisema Rais Samia baada ya kupokea ripoti ya CAG, TAKUKURU

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itafanyia kazi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

Habari za SiasaTangulizi

Deni la Serikali laongezeka kwa trilioni 11

Spread the loveDENI la Serikali imeongezeka kwa takribani Sh. 11 trilioni sawa...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

error: Content is protected !!