September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Rais Magufuli achukue hatua za muda mrefu’

Spread the love

KAZI inayofanywa na Rais John Magufuli ya kutumbua majibu inaelezwa kuwa na manufaa endapo tu, hatua hizo zitakuwa za muda mrefu, anaandika Pendo Omary.

Ruth Hiyob Mollel, Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Ofisi ya Rais (Utumishi) amesema, Rais Magufuli anapaswa kuangalia hatua zaidi ili kuhakikisha majipu hayo hayaoti tena.

Amesema, hatua hiyo ndiyo inayoweza kuakisi kwamba amepambana na ufisadi ambao ulikuwa umeota mizizi nchini.

Akizungumza na mtandao huu Ruth ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) amesema, “hatua ya Rais Magufuli ya kutumbua majipu ni sawa lakini hatua hiyo iwe ni ya muda mrefu.”

“Kufukuza tu haitoshi, lazima ufumbuzi wa muda mrefu kwamba viongozi na watumishi wa umma wafanyiwe uchunguzi na upekuzi kabla ya kuteuliwa,” amesema Ruth.

Soma mahojiano kamili na mbunge huyo katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

error: Content is protected !!