Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli achimba mkwara kiaina
Habari za Siasa

Rais Magufuli achimba mkwara kiaina

John Magufuli, Rais wa Tanzania akihutubia katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru
Spread the love

RAIS John Magufuli, amesema mtu yeyote atakayejitokeza na kujaribu kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zazibar atavunjika yeye, anaandika Dany Tibason.

Amesema kuulinda Muungano si jambo rahisi,kwani baadhi ya nchi zilijaribu kuwa na muungano lakini hazikufanikiwa.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana wakati wa sherehe za miaka 53 ya Muungano ambayo kwa mara ya kwanza zimefanyika mjini hapa.

“Kuulinda muungano si jambo rahisi, kulinda ndoa tu imekuwa vigumu, hivyo tuwashukuru waasisi wetu Mwalimu Nyerere na Abeid Karume kwa mchango mkubwa waliotoa na kufanikisha kuwa na muungano huu,” amesema Magufuli.

Amesema Muungano huo umekuwa na mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa, licha ya kuendelea kuwapo kwa changamoto ambazo zinaendelea kufanyiwa na kamati ya pamoja iliyopo chini ya Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu.

‘Leo Mama Maria na Mama Karume wapo, tunawashukuru sana. Pia nawapongeza viongozi waliotangulia kuanzia awamu ya pili hadi ya nne. Ninachoweza kuwaahidi mimi na Dk Shein (Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein) tutafuta nyayo zenu katika kuulinda Muungano,” amesema.

Amesema maadhimisho hayo ni makubwa na kwamba wananchi wanapaswa kuyatumia kwa kutafakari tulipotoka, tulipo na tunapokwenda huku akisema ni jukumu la kila mmoja kuulinda Muungano bila kujali itikadi za vyama, kabila.

Amesema ili kuuenzi Muungano kwa vitendo, wananchi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii

Rais John Magufuli aliwasili katika uwanja wa Jamhuri saa 3: 15 na kupanda katika gari la wazi akiwa na Mkuu wa Majeshi, Vanance Mabeho.

Alipita uwanjani na kusalimia wananchi  na baadaye kupata heshima ya rais kwa kupigiwa mizinga 12 na kisha kushuka kwenye jukwaa na kwenda kukagua gwaride.

Baadaye gwaride lilipita mbele  ya Rais kwa mwendo wa polepole na mwendo wa haraka.

Hii mara ya kwanza kwa mara ya kwanza maadhimisho ya Muungano kufanyika mjini Dodoma. Haya ni maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Katika sherehe hizo Marais wastaafu waliweza kuhudhuria huku baadhi ya wastaafu wengine hawakuweza kuonekana katika sherehe hizo.

Marais wastaafu ambao waliweza kufika katika asherehe hizo ni pamoja na Rais wa awamu ya pili Ally Hasan Mwinyi pamoja na wake zake waili walihudhuria huku rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete naye alikuwepo.

Pamoja na wastaafu hao kuwepo lakini rais mastaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa hakuonekana katika maonesho hayo wala mke wake.

Kwa upande wa mawaziri waku wastaafu ni waziri mstaafu Mizengo Pinda pekee ambaye aliweza kuhuduria sherehe hizo huku, mawaziri wakuu kama Fredrick Sumaye, Edwarld Lowasa, Dk. John Malecella na Jaji Joseph Warioba wakiwa hawaonekani.

Kwa upande wa maspika wastaafu aliweza kuonekana Anne makinda pamoja na wake za waasisi wa muungano huo Mama Maria Nyerere pamoja na Fatuma Karume.

Kwa upande wa viongozi wa kisiasa viobgizi wote wa vyama vya upinzani na vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi hawakuudhuria sherehe hizo huku wabunge wa upinzani vyama vyote wakishindwa kuhudhuria sherehe hizo huku wabunge wa CCM wakiwa peke yao katika sherehe hizo.

Sherehe hizo zimepambwa na vikundi mabalimbali vya burudani huku vikosi mbalimbali vya majeshi ya Tanzania vikitoa burudani zaidi.

Kwa upande wa burudani kikundi cha makomandoo kilionekana kuwa kivutio zaidi huku haraiki ya watoto ambayo iliandaliwa maalumu na mkoa wa Dodoma kwa maana ya kufanya gwaride, na kutoa heshima kwa rais.

Vikundi vingine ni kikundi cha ngoma cha Mchoya kutoka Dodoma,kikundi cha ngoma kutoka Pemba, Yamoto Band pamoja na kwaya kutoka Makongoro jijini Mwanza.

Pamoja na hayo yote baadhi ya wananchi wamelalamikia wamelalamikia kitendo cha kutoruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi licha ya kueleza kuwa waliwahi kufika uwanjani hapo.

Mmoja wa wananchi aliyezungumza na Tanzania daima alisema walitamani sana kuingia uwanjani kujionea jinsi vikundi vya burudani lakini wamekosa fursa hiyo kutokana na kuzuiliwa kuingia ndani jambo ambalo limewafanya kujisia vibaya.

Juma Khamisi ni kati ya wananchi ambao walizungumza na Tanzania daima kwa kuewleza kuwa alijitahidi kuwahi uwanjani hapo lakini hakupata bahati ya kuingia uwanjani na kusababisha anyeshewe na mvua.

Sherehe za Muungano zimefanyika kwa mara ya kwanza mkoani Dodoma,huku yakiwepo matarajio kuwa sherehe hizo zitakuwa zikifanyika kila mwaka mkoani Dodoma. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Hatutazuia watu kuingia barabarani

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kuruhusu vyama...

error: Content is protected !!