Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli aahidi maumivu kwa wapinzani
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli aahidi maumivu kwa wapinzani

Dk. John Magufuli, Rais wa Tanzania
Spread the love

RAIS wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli, ameahidi maumivu kwa vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam …(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Januari 2020, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watendaji wa chama hicho na jumuiya zake za mikoa na wilaya.

Amesema, ushindi wa zaidi ya asimilia 90 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2019, ni dalili tosha kwamba CCM itapata ushindi wa kutosha kwenye uchaguzi huo.

“Kwa namna ya pekee nawapongeza kwa kupata ushindi wa kishindo wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi Novemba 2019 ambapo CCM ilishinda kwa zaidi ya silimia 90, natambua kwa asilimia kubwa umetokana na jitihada zenu kwa kuchagua wagombea wanaokubalika,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

“Lakini hii pia ni dalili nzuri kwa chama chetu katika uchaguzi wa mwezi Oktoba hao, wengine wataendelea kuisoma namba. Na haya ndiyo matumaini yangu.”

https://youtu.be/m1PLZTSsOTY

Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli amesema chama chake hakitaomba matajiri fedha za kugharamia kampeni za.

Dk. Magufuli amewataka watendaji hao kuhakikisha wanasimamia vyema mali, rasilimali na miradi ya CCM ili kuongeza mapato, kwa ajili ya kukiwezesha chama hicho kugharamia shughuli mbalimbali, ikiwemo kampeni za uchaguzi.

Amesema kutegemea fedha za misaada kutoka kwa matajiri, kulipelekea baadhi ya matajiri kujimilikisha chama hicho.

“Na kwa mwelekeo huu nina uhakika mapato ya chama yataendelea kuongezeka kwa kasi na tutaweza kugharamia shughuli mbalimbali za chama ikiwemo kampeni za uchaguzi mkuu.

Hatutaki chama kikubwa kama hiki kiendelee kuwa ombaomba na kutegemea matajiri wachache ambao baadae hujimilikisha chama na kuweka mfumo wao, nawahakikishia sitaruhusu itoke kwenye uongozi wangu,” amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amesema zoezi la uhakiki na urejeshaji wa mali na rasilimali za CCM, umepelekea mapato ya chama hicho kuongezeka kutoka Sh. 41.1  bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2015/16 hadi Sh. 59.8 bilioni mwaka 2018/19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!