August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Maduro agoma kung’olewa

Spread the love
SERIKALI ya Venezuela imefuta mpango wa kupiga kura ya maoni kumwondoa Nicolas Maduro, rais wa nchi hiyo kutokana na kudorora kwa uchumi wa nchi hiyo, anaandika Wolfram Mwalongo
Maduro amesabisha anguko la bei ya mafuta huku nchi hiyo ikitegemea asilimia 96 ya pato lake katika sekta hiyo huku uhaba wa chakula ukinyemelea taifa hilo kutokana na mfumko wa bei uliofikia silimia 180.
Hata hivyo kiongozi huyo anatuhumiwa kushindwa kukutana na raia wake ili kunusuru mapigano yaliyoibuka tangu kuanguka kwa bei ya mafuta nchini humo.
Kufutia hali hiyo jumuhiya ya nchi za Amerika kupitia kwa Luis Almagro katibu mkuu wa umoja huo(OAS) amemwandikia barua inayo mwonyesha kiongozi huyo ni dikteta kutokana na kukwepa kukutana na raia wake pamoja na kuwazuia kufanya maamuzi wayatakayo.
error: Content is protected !!