January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kikwete mtegoni tena

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa TCD

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa TCD, mara baada ya mazungumzo yao Ikulu ndogo mjini Dodoma

Spread the love

BAADA ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukwama kufanya kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa 30 Aprili mwaka huu, sasa wadau wa demokrasia wanambana atekeleze makubaliano baina yake na vyama vya siasa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mara mbili mwaka jana kati ya Agosti na Septemba, Rais Kikwete alikutana na kujadiliana na viongozi wa vyama vya upinzani vyenye wabunge kupitia Kituo cha Demokrasia nchini (TCD).

Katika kikao hicho, ilikubaliwa kuwa muda wa kufanyika kura ya maoni usingetosha, hivyo Katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya 1977, ni muhimu kuifanyia mabadiliko kidogo pamoja na sheria ya uchaguzi yatakayowezesha nchi kufanya uchaguzi huru na haki.

Hata hivyo, katika hatua ya kushangaza 8 Oktoba mwaka jana, wakati akikabidhiwa Katiba inayopendekezwa, Rais Kikwete aligeuka makubaliano hayo na kuwataka wananchi wajiandae kwa kura ya maoni.

Hali hiyo iliibua mtafaruku mkubwa kwa wadau wakihofia uchaguzi mkuu kufanyika katika mazingira yasio huru na haki na hivyo kutoa mwanya wa uchaguzi kuvurugwa na vile vile wananchi wasiokuwa na vyama kukosa haki ya kuchaguliwa.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, waliafikiana kuwe na Tume huru ya uchaguzi,
mshindi wa uchaguzi wa Rais ashinde kwa zaidi ya asilimia 50 (50% +1),
matokeo ya Rais kupingwa mahakamani na kuruhusu mgombea binafsi.

Hivi karibuni NEC iliongeza ugumu, hii ni baada ya kutangaza kuahirisha tarehe ya Aprili 30 mwaka huu, kuwa ya kupiga kura ya maoni. Sababu kubwa ni kutokamilika uandikishaji wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR.

Tangu kuanza kwa kazi hii takribani miezi miwili, NEC haijafanikiwa kumaliza kuandikisha hata mkoa mmoja wa Njombe. Hii ni kutokana na kutopatiwa fedha ya kutosha kununulia vifaa.

Kutoka na hali hiyo, wadau wa demokrasia sasa wanapendekeza na kumshawishi Rais Kikwete, ageukie kutekeleza kile alichokubaliana na vyama vya siasa ili kulinusuru taifa liingie kwenye uchaguzi na mgawanyiko.  

Hebron Mwakagenda – Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), ameliambia MwanaHALISIOnline, kuwa “Serikali inapaswa kutekeleza makubaliano ya Chamwino kati ya Rais Kikwete na TCD”.

Anasema “Mchakato wa kupata Katiba Mpya hauna baraka. Kwa sasa serikali inapaswa kutekeleza makubaliano ya Rais na TCD hata kwa hati ya dharura katika Bunge lijalo.”

Mwakagenda amesema, licha ya NEC, kuhairisha tarehe ya kura ya maoni 30 Aprili na kutangaza kufanyika baada ya Julai mwaka huu, itakuwa ni kulazimisha kinyume na matakwa ya wananchi wengi.

“Katiba inayotakiwa kupigiwa kura ya maoni inakataliwa na makundi mbalimbali. Sio haki kutumia fedha za umma kwa jambo ambalo haliwezekani kwa mwaka huu. Kwa sasa uchaguzi mkuu ni muhimu kuliko kura ya maoni,”Mwakagenda amefafanua.

error: Content is protected !!